| Hip
hop yaenguliwa tuzo za Kili!
Muziki
wa hip-pop umeondolewa katika mashindano ya
mwaka huu ya tuzo ya mwanamuziki bora, Kili
Music Awards, yatakayoanza mwishoni mwa mwezi
huu katika ngazi za kanda na fainali kufanyika
Mei.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, ambao ndio wadhamini
wa mashindano hayo, Oscar Shelukindo alisema
jijini juzi wakati wa uzinduzi wa mashindano
kuwa muziki huo umeondolewa kutokana na kuwa
vigumu kupata albamu iliyokamilika.
Hata hivyo, Shelukindo alisema pamoja kwa kuondolewa
muziki huo, mashindano ya mwaka huu yatashirikisha
aina 24 za muziki, ambazo zipo zilizoongezwa
kutokana na kuonekana kuwa na ushindani.
``Mambo mengi ya mchanganuo wa mashindano tutatoa
baadaye wiki ijayo ila tu mwaka huu tutakuwa
na categories nyingi tofauti na mwaka jana,?
alisema Shelukindo.
Alisema mwaka huu kutakuwa na kanda nne ambazo
ni Kaskazini, Kusini, Ziwa na Kati, ambazo washiriki
wake watapambana na kupatikana kwa mshindi mmoja
atakayekuja ngazi ya taifa kwa kila aina ya
muziki.
Alisema kampuni ya bia nchini, TBL, itaendelea
kudhamini mashindano hayo kwa kipindi cha miaka
mitano ijayo kuanzia mwakani, baada ya kumaliza
kipindi kama hicho mwaka huu.
``Kampuni inatumia zaidi ya milioni 200 kwa
mwaka kwa ajili ya mashindano haya, hivyo tumeongeza
miaka mingine mitano kwa ajili ya kuendesha
mashindano haya, ambayo yanatoa fursa kwa wasanii
wa Tanzania kuonyesha vipaji vyao,`` alisema.
Pia alisema tuzo hizo zitaboreshwa ili ziweze
kutambuliwa kwa Afrika Mashariki na Kati, kwa
msanii aliyepata kuweza kupambanishwa kutokana
na sifa na ubora wake, pia washindi wataendelezwa
kwa kupata programu za maendeleo ambapo watashirikiana
na Baraza la Sanaa la Taifa, (BASATA).
Naye mwakilishi kutoka BASATA, Anjelo Luhala
alisema TBL kupitia tuzo hiyo inaendeleza sera
ya utamaduni ya mwaka 1997, ambapo tayari wamewawezesha
wanamuziki 120 kupata tuzo hizo kutokana na
kazi zao.
Luhala alisema sasa muziki wa Tanzania umekua
na kujulikana nchi mbalimbali na kufanya kazi
za wasanii kupata soko kubwa.
``Tunachukua fursa hii kuwapongeza TBL kwa
kuwawezesha wasanii wa Tanzania muziki wao kuwa
na soko ambalo linaongeza kipato chao, `` alisema
Luhala.
Hata hivyo, aliwataka wasanii hao kubadilika
kwa kujiendeleza katika taaluma ya muziki, pia
wawe wajasiriamali kwa kujijengea mitaji na
kuanzisha vikundi vya Saccos na wajue haki zao
zinazolinda maslahi ya kazi zao, kuepuka kulanguliwa
na watu wasiopenda maendeleo yao, kwani ulimwengu
wa sasa hauendi kwa kubahatisha.
Mpigie kura msanii au bandi uipendayo PIGA KURA SASA!!!!! |