WASHINDI WA TUZO ZA KILI 2010 WAPATIKANA!
Mshindi wa tuzo ya Mwanamuziki Mashuhuri na Wimbo Bora wa Mwaka katika Tuzo za Muziki za Kilimanjaro kila mmoja atazawadiwa Sh milioni moja imebainika.
Tamasha la kutoa tuzo za KILI 2010 lilifanyika tarehe 14 May 2010 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo washindi 22 walipatikana. Tukio hilo lilioneshwa (Live) moja kwa moja na kituo cha televisheni cha TBC 1 na kuhudhuriwa na watu mashuhuri nchini, wasanii wote waliochaguliwa kuwania tuzo na wadau wa muziki.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro waandaaji wa tamasha hilo, George Kavishe alisema jana kwamba zawadi za fedha taslim kwa washindi wa makundi mengine zilitolewa siku ile ile wakati wa kukabidhiwa tuzo zao.
Kilimanjaro Premium Lager imefikisha muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio.
It's Tanzanian Time, Make the most of It!
SEAN KINGSTON ATEMBELEA KIWANDA CHA BIA CHA TBL!!
Mwanamuziki Sean Kingston Kutoka Marekani alisaini kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Tanzania Breweriers, Bw. David Minja pichani. Sean Kingston atashiriki katika utoaji wa tuzo za wanamuziki bora wa mwaka 2009/2010 kwa ajili ya kukabidhi tuzo za Kiliamanjaro Music Award lakini pia atafanya onyesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee pamoja na washindi wa tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa kesho kwenye ukumbi huohuo.
Mwanamuziki Sean Kingston kutoka Marekani aliwambia waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika Hoteli ya Dubble Tree Hilton Jijini Dar es salaam leo wakati alipozungumzia ujio wake katika kushiriki kwenye utoaji wa tuzo za Kilimanjaro Music Award utakaofanyika kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na kufuatiwa na onesho kubwa jumamosi akishirikiana na washindi mbalimbali wa tuzo za kilimanjaro Music Award, kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL David Minja.
SEAN KINGSTON LIVE IN DAR ES SALAAM.
Kilimanjaro Premium Lager inawaletea Sean Kingston live in Dar, ataonekana kwenye usiku wa tuzo za Kili 2010 tarehe 14/05/2010 akiwapa suport washindi wa Killi Music Awards, na tarehe 15/05/2010 ndani ya Diamond Jubilee, Sean Kingston atashuka dimbani na washindi wa 2010 killi Music Awards kwa show moja tu live na Bendi yake nzima kutoka States kwa Kiingilio cha shillingi 15,000 Tu Kwa Ticket za awali.
Ticket zitaanza kuuzwa siku 5 kabla ya concert na vituo vitatajwa hapo baadae. Kwa wale watakao nunua Ticket Mlangoni Zitapatikana kwa shillingi 20,000 Tu. Kutakua na interviews za moja kwa kwa moja ndani ya studio tofauti na sean Kingston Kabla ya siku ya Tunzo.
IT'S TANZANIAN TIME, MAKE THE MOST OF IT |