Picture Gallery Send us feedback

NEWS

Kanda Zaidi Kili Music Awards mwakani!

Mashindano ya tuzo za wanamuziki bora za Kilimanjaro nchini mwakani zitashirikisha kanda zaidi ili kuvumbua vipaji vya wasanii chipukizi. Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo, Oscar Shelukindo alisema jijini juzi kwenye seminar ya nominees kuwa kanda hizo zitaongezwa kutoka nne na kuwa zaidi. Shelukindo alisema lengo kubwa la wadhamini, ambao pia ndio waandaji wa mashindano hayo ni kuhakikisha sanaa ya muziki nchini inakuwa juu, kutokana na wasanii wengi chipukizi wanatokea kwenye kanda. " Katika kanda kunawanamuziki wengi sana wa kizazi kipya ndio maana baada ya fainali za mashindano mwaka huu tutakaa na kupanga mikakati ya kuongeza kanda zaidi kwa mwakani," Alisema Shelukindo.

Washindi wa kanda wa mwaka huu katika muziki wa kizazi kipya na nyimbo za asili ni Macy Simon na MWanza Sanaa (Kanda Ziwa), Contiguous na JKT Oljoro ( Kaskazini), Connection na Hiyari ya Moyo (Kati) na Mashada Hewani na Mbeya Community Development Organisation (Kusini). Hatahivyo, TBL, juzi iliandaa semina ya siku moja kwa wasanii waliotangazwa kushindanishwa katika muziki wa aina mbalimbali, ambapo walifundishwa namna ya mshindi anavyopatikana kwa kupigiwa kura za kukata kupuni kwenye magazeti, utuma ujumbe mfupi kwenye simu ya mkononi na kutumia mtandao wa tovuti. Pia wasanii hao wapatao 150 walipata fursa ya kuuliza maswali kwa majaji, ambao baadhi yao wanatoka kwenye Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA, pia walipata mafunzo ya utaratibu mzima wa kujiunga na huduma ya benki ya Wananchi Dar es Salaam, ambapo wanaruhusiwa kukopa lakini kwanza wawe na akaunti katika benki hiyo.

Meneja wa tawi la Arnatouglu, Cascilas Slyvesta aliwataka wasanii kufungua akaunti ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kupata fedha za kurekodia kazi zao hata kununua vifaa vya muziki.

Mpigie kura msanii au bandi uipendayo PIGA KURA SASA!!!!!

 
Habari zaidi