Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetangaza udhamini wa Shilingi
milioni 20 kwa mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo zimepangwa
kufanyika February 28, 2010 Mkoani Kilimanjaro.
Akitangaza udhamini huo jana, meneja wa bia ya Kilimanjaro,
Bw. George Kavishe alisema udhamini huo ni sehemu ya jitihada
za kampuni yake kusaidia maendeleo ya michezo nchini na
kwamba zawadi za msimu ujao zitaongezeka mara dufu.
Bw. George Kavishe, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro
"Tumeongeza fedha hadi kufikia milioni 20, kiwango
ambacho ni kikubwa kutolewa kama zawadi katika mashindano
yote ya riadha hapa nchini.
"Natumaini ongezeko la zawadi litawapa moyo wanariadha
wetu na kufanya vizuri zaidi katiak mashindano hayo na kuvunja
rekodi zilizopo ili waweze kupata nafasi ya kushiriki mbio
kubwa zaidi za kimataifa,"alisema Shelukindo.
Alisema mchezo wa riadha ndio mchezo pekee ulioiletea Tanzania
sifa kubwa kwenye anga za kimataifa na akaongeza kuwa ushirikino
kati ya kampuni yake na chama cha riadha utasaidia kuboresha
viwango vya riadha nchini.
TBL imekuwa ikidhamini mashindano hayo tangu mwaka 2003
na mwaka jana yalishirikisha washiriki 35,000 kutoka sehemu
mbalimbali duniani.
Naye mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali
Idd Kipingu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo
aliishukuru TBL kwa kutoa mchango mkubwa katika kuendeleza
riadha nchini.